Jumatatu , 19th Sep , 2022

Mwili wa Malkia Elizabeth II utapumzishwa hii leo Septemba 19, 2022, baada ya siku kadhaa za kuaga.

Malkia Elizabeth II

Mwili huo utasafirishwa kwenda Westminster Abbey kwa ibada ya kidini mbele ya maelfu ya watu, na kisha kupelekwa Kasri la Windsor kwa ibada ya kifamilia na watu wa karibu na hatimaye kuzikwa kibinafsi.

Malkia Elizabeth II alifariki dunia Septemba 8, 2022, akiwa na umri wa miaka 96.

Wakuu wa nchi kutoka kote ulimwenguni wamekuwa wakiwasili kuungana na washiriki wa familia ya Kifalme kukumbuka maisha na huduma ya Malkia.