Jumatatu , 25th Mar , 2024

Takwimu zinazonyesha asilimia kubwa ya vifo vyote duniani vinasababishwa na ajali ambazo mara nyingi huchangiwa namakosa ya binadamu kushindwa kufuata kanuni za barabarani.

Dkt. Prosper Mgaya, Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji nchini (NIT)

Akizungumza na wadau wa usafirishaji kutoka Mikoa ya Mwanza, Geita na Mara, Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji nchini (NIT) Dkt. Prosper Mgaya amesema katika kuhakikisha usalama unaimarika chuo hicho kinakutanisha wadau wa usafirishaji ili kuweka mikakati ikayosaidia kumaliza tatizo hilo.

Aidha, Dkt. Mgaya amebainisha kuwa ipo haja ya kutafuta mwarobaini wa ajali hizo ambazo zinapunguza nguvu kazi ya taifa.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Ilemela Hassan Masala amekitaka chuo hicho kuendelea kutoa mafunzo kwa wasimamizi wa  sheria za usalama barabarani ili kusaidia kupunguza ajali za barabarani.