Shekhe Mussa Kundecha, Amiri Mkuu Baraza kuu la Jumuiya ya taasisi za Kiislam.
Vijana wengi ukiwatajia suala la kuoa wamekuwa na malalamiko mengi kuhusu ukubwa wa mahari na wengine wakitengeneza vibonzo kuwa wazee wapunguze mahari, je mahari hasa ni nini?
"mahari ni makubaliano baina ya familia ya muoaji kwenda kwenye familia ya mwanamke, pili ni zawadi kutoka kwa mwanaume kwenda kwa mwanamke anayemuoa na wazazi hawatakiwi kuchukua mahari, labda mwanamke aamue kuwapa wazazi wake lakini", alisema Shekhe Mussa Kundecha, Amiri Mkuu Baraza kuu la Jumuiya ya taasisi za Kiislam.
"Kuna wazazi wamegeuza watoto wa kike kama mtaji wa kujipatia mali wengine wanaenda mbali zaidi kuwa mabinti weupe Mahari zao kuwa kubwa zaidi kitu ambacho wanakosea na kusababisha vijana wanaogopa kuoga na kusababisha wengine wanazeeka bila kuoa wala kuolewa", alisema Mchungaji Thomas Muyya-Mkurugenzi Baraza la Dini mbalimbali.
Hiyo ni kwa upande wa Dini, je kimii Mahari inatakiwa kuwaje?
"Mahari inatakiwa wapenzi wakubaliane kwanza mwanamke amuulize mwanaume wake anaweza kulipa kiasi gani kisha anaenda kuwaambia wazazi wake atakapokuja kutoa Mahari wasimzidishie ili ndoa iweze kufungwa, japo wazazi wengine huwa chanzo cha kuwawekea watoto wao Mahari kubwa kitu ambacho wanakosea", alisema Hadija Shebila Somo.
Vijana nao wana lipi kuhusu kuoa?
"Mahari chanzo sana cha kutukwamisha kuoa kwa maana vijana bado tunajitafuta bado bado hatuna maisha mazuri, kuna jamaa mmoja alighairi kuchukua mke eti wanamnyima mke kisa hajamalizia mahari", alisema Hassan Machupa Kijana.
"Maisha magumu unataka kuoa unaambiwa Mahari milioni 2 kama unataka kununua nyumba ukiangalia kipato chako kupala tu laki moja ni mtihami tutawezaje kulipa mahari zote hizo", alisema Said Kapomo, Kijana.