Jumatano , 20th Oct , 2021

Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini Wilbroad Mutafungwa, amesema magari yatakayofanyiwa ukaguzi katika maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama yatawekewa stika maalum na jina la Askari aliyelifanyia ukaguzi kwa lengo la kuepusha janja janja ya madereva wenye magari mabovu.

Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Wilbroad Mutafungwa

Kauli hiyo ameitoa hii leo Oktoba 20, 2021, wakati akizungumza kwenye kipindi cha Supa Breakfast cha East Africa Radio, katika kuelekea maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama barabarani ambayo yatafanyika mkoani Arusha yenye kauli mbiu isemayo, “Jali Maisha Yako Na Ya Wengine Barabrani”.

"Katika maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama, gari ikikaguliwa itawekwa sticker maalum itakayoonesha kwamba hili gari limeshakaguliwa na pia gari litawekwe bampa sticker ya ujumbe wetu wa mwaka huu, kwa lengo la madereva kujikumbusha," amesema Kamanda Mutafungwa