Jumatatu , 15th Nov , 2021

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi, amewapiga marufuku madalali wa nyumba wanaochukua kodi ya mwezi mmoja kwa wapangaji na badala yake pesa hizo walipwe na wenye nyumba.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi

Kauli hiyo ameitoa hii leo Novemba 15, 2021, mkoani Iringa na kusema kwamba kitendo cha kuchukua pesa kwa mtu anayepanga ni wizi wa waziwazi.

"Tunawashangaa hawa majambazi wanaochukua kodi ya mwezi kwa mpangaji, hawa madalali wanaochukua pesa kwa mpangaji waache mchezo huo kwa sababu ni wizi wa mchana kabisa, mwenye nyumba lazima akulipe wewe," ameeleza Waziri Lukuvi 

Tazama video hapa chini