Jumamosi , 21st Jun , 2014

Maabara kubwa tatu nchini Tanzania leo zimekabidhiwa hati ya ubora na nchi za jumuiya ya maendeleo kusini mwa Africa SADC pamoja na taasisi mbalimbali za kimataifa ambapo maabara hizo sasa zitakuwa zikitoa huduma kwa kiwango cha kimataifa.

Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii,Seif Rashid

Maabara kubwa tatu nchini Tanzania leo zimekabidhiwa hati ya ubora na nchi za jumuiya ya maendeleo kusini mwa Africa SADC pamoja na taasisi mbali mbali za kimataifa ambapo maabara hizo sasa zitakuwa zikitoa huduma kwa kiwango cha kimataifa.

Akipokea hati hizo waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Seif Rashid amezitaja maabara hizo kuwa ni ile ya taifa iliyopo taasisi ya utafiti wa magonjwa ya binadamu NIMR, Maabara ya Bugando ya jijini Mwanza pamoja na maabara ya mkoa wa Mbeya.

Dk. Rashid amesema kupitia maabara hizo sasa zinaweza kutumika kimataifa kwa kupima vipimo mbalimbali vya magonjwa badala ya kutumia maabara nyingine za nje ya nchi pale panapohitajika kupatikana kwa majibu ya ugonjwa fulani.