Said Lugumi akiongea na waandishi wa habari alipo waalika watoto yatima.
Watanzania wameomba kuwakumbuka watoto wanaoishi mazingira magumu ili na wao waweze kusherehekea kama ambavyo watoto wanaoishi na wazazi wao wanafurahia.
Hayo yamesemwa na baadhi ya wasamaria wema jijini Dar es Salaam ambao siku ya leo wamesherehekea sikukuu ya Noel na watoto yatima ili kuwarudishia faraja ya kutoishi na wazazi wao.
“Sio kila mtu ana moyo wa kuwakumbuka watoto wanaoishi nazingira hatarishi lakini tukipata neema kwa pamoja tushirikiane kupunguza changamoto zinazowakabili katika maisha yao”, SAID LUGUMI-Msamsria mwema
Kwa upande wao wasimamizi wa vituo vya kulelea watoto yatima wameshukuru wasamaria wema kuwakumbuka katika sikukuu hii huku wakielezea changamoto wanazokabiliana nazo.
“Tunashukuru sana leo tumesherehekea sikukuu kwa kupata makazi ya kudumu tulikuwa tumepanga lakini sasa hivi tutaishi kwenye nyumba zetu tunaomba na wengine waweze kuguswa na watoto wanaoishi mazingira magumu”, AISHA SUDI-Msimamizi wa kituo.
"Tunashukuru tunavyopata misaada kama hii inasaidia sana kurudisha furaha kwa watoto tunaowalea kwani hawana wazazi na tunaomba watu wengine waweze kuguswa na kusaidia watoto wanaoishi kwenye mazingira hatarishi", HAJI MAHMOUD-Msimamizi wa kituo
Mfanyabiashara Saidi Lugumi leo Disemba 24, 2024 amesherehekea sikukuu hii kwa kupata chakula nao pamoja na kuwakabidhi jengo kwa ajili ya makazi ambapo hapo awali walikuwa wakiishi katika nyumba za kupanga.
“Nakabidhi nyumba moja leo lakini ninejenga nyumba nyingine sita kama hii kwa ajili ya kuwasaidia watoto yatima wanaoishi katika vituo vya kulelea watoto”, SAID LUGUMI-Msanariamwema.