Ijumaa , 2nd Oct , 2020

Mgombea wa Urais kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo,(CHADEMA), Tundu Lissu, amepinga uamuzi wa Tume ya tiafa ya Uchaguzi na kusema kuwa ataendelea na mikutano yake ya kampeni siku ya jumapili.

Mgombea wa Urais kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo,(CHADEMA), Tundu Lissu.

Akizungumza na waandishi wa habari leo nyumbani kwake Tegeta Lissu ameweka wazi kuwa hatofuata uamuzi wa Tume wakumtaka kutokufanya kampeni kwa siku saba kuanzia tarehe 3/10/2020.

"Kamati kuu ya chama chetu inakutana kesho ili kulijadili suala hili na kulitolea ufafanuzi,msimamo wangu binafsi ni kwamba kampeni zinaendele siku ya jumapili kama mabavyo imepangawa kwenye ratiba iliyoratibiwa na tume ya taifa ya uchaguzi kwa hiyo msimamo ndio huu" amesema Lissu

Aliendele kusema kuwa, "Mimi najiandaa kwa mikutano ya kampeni siku ya jumapili, kamati kuu ndiyo itatokayo toa uamuzi mimi najianda kwa kampeni kesho kutwa".