Ijumaa , 8th Apr , 2016

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon, amesema kuwa njia bora ya kuhakikisha kutotokea tena kwa mauaji ya kimbari na ukiukwaji mwingine mkubwa wa haki za binadamu, ni kutambua wajibu wa pamoja na kuwalinda walio hatarini.

Balozi Eugène-Richard Gasana Rwanda

Katika taarifa ya ujumbe wake wa siku hiyo, Ban amesema kuwaenzi wahanga wa mauaji ya kimbari pia kunamaanisha kufanya juhudi za kuendeleza haki na uwajibikaji.

Amepongeza nchi wanachama katika kanda ya Maziwa Makuu na kwingineko, kwa juhudi zinazoendelea za kuwakamata na kuwapeleka mbele ya sheria watoro waliosalia, ili kukomesha ukwepaji sheria.

Balozi Eugène-Richard Gasana Rwanda, ni mwakilishi wa kudumu wa Rwanda katika ofisi ya Umoja wa Mataifa mjini New York amewataka Wanyarwanda kushirikiana kwa pamoja na kufuta fikra zote za yaliyotokea awali na kuhakikisha mauaji hayo hayatokei tena.