Amesema kituo hicho huenda kikawanyima watanzania fursa za ubunifu na fikra mbalimbali za watanzania katika kuendesha na kumiliki viwanda hasa vile vidogo.
Ameyasema hayo jijini Dar es salaam kwenye kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda na Biashara na kuongeza kuwa serikali ifikirie njia nyingine ya kubuni biashara inayokaribiana na uendeshaji wa kituo hicho.
Mheshimiwa Lema ameongeza kuwa sambamba na hilo la uwekezaji serikali ipitie upya riba mbalimbali zinazotakiwa kulipwa na wafanyabiashara pindi wanapokopa pesa kwaajili ya kufanyia biashara zao kwenye mabenki mbalimbali na taasisi mbalimbali za kifedha.
Amezishauri Wizara ya Fedha na Mipango na Wizara ya Viwanda na Biashara kuangalia utaratibu mpya wa kuboresha huduma za kifedha nchini.






