Jumatatu , 2nd Mei , 2016

Mkoa wa Pwani umekumbwa tena na mlipuko wa Ugonjwa wa kipindupindu katika maeneo mbalimbali ya mkoa huo baaada ya kudhibitiwa kwa kipindi hca wiki mbili zilizopita.

Mkuu wa mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo,

Mkuu wa mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo, amekiri ugonjwa huo kulipuka upya katika maeneo ya Mlandizi na Bagamoyo, na kuthibitish kuwa amepata taarifa ya wagonjwa wapya watatu wenye maambukizi ya gonjwa huo.

Mhandisi Ndikilo amesema kuwa licha ya mvua zinazoendelea kunyesha kwa wingi katika mkoa huo lakini pia miundo mbinu mibovu inayotuamisha maji ndio chanzo cha kusambaa kwa ugonjwa huo ikiwa ni pamoja na utupaji taka hivyo.

Mkuu huyo wa Mkoa amewataka wananchi wa Mkoa huo kuendelea kutunza mazingira ikiwemo pia kufuata kanuni za afya ikiwa ni pamoja na kunawa mikono kabla ya kula lakini pia kuacha kula hovyo vyakula vya mamalishe wanapika katika mazingira machafu.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa chama cha Marafiki wa Kongowe, Speratus Rwamgila, amesema kuwa wameakua kufanya usafi katika eneo hilo la Kongowe na hospitali ya Kongowe kutokana na kuwepo katika mazingira machafu.

Sauti ya Mkuu wa mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo.