Jumapili , 11th Mei , 2014

Wakazi wa Kinondoni B jijini Dar es salaam nchini Tanzania, wameelezea kukumbwa na hofu ya kuugua ugonjwa wa Dengue kutokana na uwepo wa maji yaliyotuama na kuzunguka nyumba katika maeneo wanayoishi hali inayosababishwa na hali duni ya miundombinu.

Wakiongea na East Africa Radio, wakazi hao wamesema ni jukumu la serikali kutengeneza miundombinu hiyo mapema ili kuwanusuru na hali ya wasiwasi waliyonayo ya kuugua ugonjwa hatari wa Dengue.

Kauli ya wakazi hao imekuja wakati ambapo takwimu za wizara ya afya zinaonyesha kuwa zaidi ya watu mia moja wameugua na kulazwa kutokana na ugonjwa huo huku wawili kati yao wakiripotiwa kufariki dunia.