Alhamisi , 10th Nov , 2016

Ripoti mpya ya shirika la mfuko wa maendeleo ya kilimo IFAD inaonesha kuwa kwa kila dola moja inayowekezwa katika mpango wa usaidizi wa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kwa wakulima wadogo ASAP, una manufaa makubwa.

Wakulima wadogo wakiwa mashambani.

Kwa mujibu wa IFAD inayohudhuria mkutano wa nchi wanachama wa mkataba wa mabadiliko ya tabianchi mjini COP22 mjini Marrakech Morocco, faida hiyo yaweza kuwa kiasi cha dola za kimarekani 1.40 na 2.60 kwa kila dola inayowekezwa, kwa zaidi ya miaka 20 ya kutekeleza makabiliano hayo.

IFAD inaamini kuwa kuwekeza kwa wakulima wadogo kutasaidia katika kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi kutokana na umuhimu wa kundi hilo katika kilimo.

Katika hatua nyingine ripoti mpya ya benki ya dunia inaonesha kuwa nchi za Afrika zinafanya vyema katika jitihada za kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi.

Benki ya Dunia imesema nchi kama vile Cote d'Ivoire na Nigeria zinatekeleza kwa mafanikio ikiwamo pia kupunguza hewa ukaa.