Akizungumza na waandishi wa habari katika eneo la tukio kanali wa jeshi Saidi Nkambi anayesimamia oparesheni hiyo amesema zoezi hilo linakwenda vizuri na tatizo linalosumbua kwa sasa ni mifuko kwa ajili ya kujaza mchanga.
Kwa upande wake kaimu mkuu wa mkoa Mtwara Ponsiano Nyama ametaka wananchi wa mikoa ya Mtwara kuwa watulivu serikali inafanya kila juhudi kuhakikisha dhoruba hiyo haileti madhara kwa mikoa ya Mtwara na Lindi, huku mhandisi wa kiwanda kilichokaribu na bahari Peter John akiishukuru serikali kwa hatua walizochukua.