Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt Hussein Mwinyi.
Waziri wa Ulinzi wa Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Hussein Mwinyi ambaye ndie alikuwa mgeni rasmi amesema maadhimisho hayo yatahusisha mazoezi ya kijeshi yenye lengo la kupima uwezo wa jeshi katika kukabiliana na maadui.
Kwa mujibu wa waziri Mwinyi, ubora wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania na nidhamu waliyonayo askari wake vinathibitishwa na ushiriki wa jeshi hilo katika operesheni mbalimbali za ulinzi wa amani ukiwemo ushiriki wa jeshi hilo katika operesheni ya umoja wa Mataifa UN nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Awali, mkuu wa Majeshi CDF Davis Mwamunyange amesema maadhimisho hayo yataenda sambamba na mazoezi ya kivita kwa shabaha za kupanga ambapo vikosi vya ardhini na angani vya jeshi hilo vitaigiza mapigano ya kivita kwa shabaha ambazo hazitakuwa na madhara.
Mazoezi hayo yatakayofanyika Monduli Arusha, yatakaongozwa na mkuu wa kamandi ya askari wa ardhini Meja Jenerali Salum Kijuu.