Ijumaa , 30th Apr , 2021

Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Meja Jenerali Charles Mbuge, amewataka vijana waliochaguliwa kujiunga na mafunzo ya JKT kwa kujitolea kwa mwaka 2020/2021 na kurejeshwa nyumbani mwezi Februari mwaka huu kurejea makambini.

Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Meja Jenerali Charles Mbuge

Kaimu mkuu wa utawala wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Kanali Hassan Mabena, amewaambia wanahabari kuwa vijana hao wanatakiwa kuripoti kwenye makambi waliyopangiwa awali.

Aidha Kanali Mabena amesema kuwa kuwa JKT wameingia makubaliano na Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) kwa ajili ya vijana kupata elimu ya vitalu.

Mwezi Februari mwaka huu, Mkuu wa  Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) alitangaza kuwarejesha nyumbani zaidi ya vijana 12,000, hadi ambapo wangetangaziwa tena.