
Mkuu wa mkoa wa Tanga, Luteni mstaafu Chiku Galawa
Akizungumza baada ya chama cha ushirika wa korosho Tandahimba na Newala kutembelea jiji la Tanga, Katibu wa chama kikuu cha ushirika wa wafugaji wa ngo'mbe wa maziwa mkoani Tanga, Athuman Mahadhi, amesema makundi ya wafugaji ambayo idadi yao kubwa ni vijana wataathirika kiuchumi kwa sababu watalazimika kusitisha shughuli zao za ufugaji walizokuwa wakifanya katika eneo hilo tangu mwaka 2000.
Bwana Mahadhi ameiomba serikali kuzingatia mpango wa matumizi bora ya ardhi kwa sababu awali iliwapatia maeneo hayo kwa lengo la ufugaji na badala yake eneo hilo ambalo linamilikiwa na kampuni ya Amboni Ltd linachukuliwa kwa ajili ya ujenzi wa makazi ya jiji la Pongwe lililopo nje kidogo mwa jiji la Tanga.