Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Felix Ntibenda.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Felix Ntibenda, wakati akipokea msaada wa madawati yaliyotengenezwa kwa kutumia mabaki ya Plastiki ikiwemo mifuko ambayo mara nyingi imekua ikichangia kuharibu mazingira.
Ntibenda amesema kuwa mpango huo wa unapaswa kuungwa mkono kwa kuwa una uwezo wa kusaidia vijana wengi zaidi mkoani humo kujipatia kipato pamoja na kupunguza uchafuzi wa mazingira jijini humo kwa kiasi kikubwa.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Green Hope Invetment iliyotengeneza madawati hayo Emmanuel Makongoro, wameamua kuitikia wito wa serikali kwa kubuni kutumia mabaki ya Plastiki ili waweze kupunguza uchafuzi wa mazingira pamoja na kusaidia vijana kupata ajira.
Kwa upande wake kijana aliepatas ajira katika kampuni hiyo Briton David, amesema mpango huo utasaidia kuyaweka mazingira ya jiji la Arusha katika hali ya Usafi.