Alhamisi , 20th Feb , 2025

Katibu Mkuu wa chama cha Alliance for Democratic Change (ADC), Innocent Gabriel Siriwa ametangaza kutia nia ya kugombea nafasi ya urais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mwaka 2025 mpaka 2030 kupitia Chama cha Alliance for Democratic Change (ADC).

Katibu Mkuu wa chama cha Alliance for Democratic Change (ADC), Innocent Gabriel Siriwa ametangaza kutia nia ya kugombea nafasi ya urais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mwaka 2025 mpaka 2030 kupitia Chama cha Alliance for Democratic Change (ADC).

 

Katibu huyo ameeleza sababu ambayo imemfanya kuwiwa kutangaza nia ya kugombea nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

 

"Nimewiwa kugombea nafasi ya urais ni kutimiza demokrasia na katika chama nimetimiza jambo la kugombea kidemokrasia na jambo la pili ni kwamba nina uwezo wakugombea na wanasiasa wengine, na naamini kwamba nikienda kwenye kampeni ninaweza kupata nafasi, na wajumbe mnaokwenda huko msisahau kwa mba Siriwa alisema ana uwezo na hapa nina vipaumbele vitano". Amesema

 

Wakati akimkaribisha mtia nia Makamu mwenyekiti wa Chama cha ADC Bara, Hassan Mvungi ameonyesha imani na mtia nia ya kugombea Urais kupitia chama cha ADC na kuwahamasisha wengine kujitokeza na kuahidi kutoa ushirikiano kwa watakao onyesha nia ya kugombea.

 

"Chama chetu cha ADC kinacho amini uwepo wa Mwenyezi Mungu na kwa kuwa viongozi wetu ambao watakuwa wanagombea kwa kuwa wataongoza vyema, lakini leo tupo hapa katika kumsupport kwa ajili ya kutia nia na wengine ambao watahamasika tunawakaribisha".

 

Nae Mwenyekiti mstaafu wa chama hicho Hamad Rashid Mohammed, amesisitiza zaidi katika uchaguzi kuhakikisha Demokrasia inafuatwa na haki inatendeka zaidi.