Jumatatu , 6th Feb , 2023

Hadi kufikia mchana wa leo, Rais wa Uturuki Recep Erdogan amesema watu 912 wamepoteza maisha nchini Uturuki pekee na wengine 5,383 wamejeruhiwa kutokana na tetemeko la ardhi.

Inasemekana zaidi ya watu 1,200 mpaka sasa wamepoteza maisha

 

Ameongeza kuwa hawezi kutabiri ni kwa kiasi gani idadi ya vifo itaongezeka wakati juhudi za utafutaji na uokoaji zikiendelea.

Hili ndilo janga kubwa zaidi nchini humo tangu mwaka 1939, Erdogan anawaambia waandishi wa habari, akiongeza kuwa majengo 2,818 yaliporomoka kutokana na hilo.

Tetemeko hilo kubwa la ardhi limetokea kusini mashariki mwa Uturuki, karibu na mpaka wa Syria na kuua mamia ya watu walipokuwa wakilala na kuwaumiza  wengine wengi.

 Idadi ya vido inaongezeka kadiri muda unavyoenda, Nchini Syria, zaidi ya watu 380 walikufa, huku waathiriwa katika maeneo yanayodhibitiwa na serikali na yanayodhibitiwa na waasi.

Wizara ya afya nchini Syria imesema watu 239 wamefariki katika majimbo ya Aleppo, Latakia, Hama na Tartus.