Ijumaa , 8th Oct , 2021

Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Mwinyi, kwa niaba ya Rais Samia leo anatarajia kupokea ndege mbili mpya aina ya Airbus zilizopewa majina ya Zanzibar na Tanzanite.

Air Tanzania

Katika ndege hizo mbili kila mojawapo ina uwezo wa kubeba abiria 132, na ina uwezo wa kuruka kwa saa 6 bila kutua, mifumo ya kuwasaidia marubani wakati wa kuruka na kutua na aina ya viti vyake ni vya tofauti ambavyo unaweza kuvibadilisha ukaaji.

Ndege hizo pia zina mifumo ya burudani ndani yake inayojumuisha burudani kwa ajili ya watoto, sinema, vichekesho na usikilizaji wa muziki wa aina mbalimbali na mitandao ya intaneti.

Ununuzi wa ndege hizo unafanya ndege zilizonunuliwa na serikali kufikia 11, na imeelezwa kwamba gharama ya ndege moja ni kiasi cha shilingi bilioni 211 za Kitanzania.