
Mkurugenzi Mtendaji HESLB - Abdul-Razaq Badru
Akizungumza katika kipindi cha EA Breakfast kinachoruka kupitia East Africa Radio, Mkurugenzi Mtendaji wa bodi hiyo Abdul-Razaq Badru amesema kuwa suala la kukusanya madeni hayo ni la kisheria hivyo bila kujali kama mdaiwa amepofariki, lazima uwepo utaratibu wa kurejesha mikopo hiyo kupitia kwa ndugu, jamaa na wadhamini wa muhusika.
Amelazimika kutoa ufafanuzi huo kutokana na kuwepo kwa majina ya watu ambao wamefariki katika orodha ya wadaiwa sugu iliyotolewa na bodi hiyo hivi karibuni.
Msikilize hapa Badru akifanya mahojiano na mtayarishaji wa kipindi cha EA Breakfast, Anna Sombida, ambapo ameanza kwa kufafanua jinsi bodi hiyo inavyowafuatilia wadaiwa sugu.