Jumatano , 22nd Jun , 2016

Ofisi ya Mwanasheria Mkuu Serikali ya Tanzania imesema kuwa serikali imeendelea kukataa suridhia suala la ushoga nchini Tanzania kati mapendekezo 72 yaliyokataliwa ya Umoja wa Mataifa kwenye mapendekezo yake kuhusu haki za binadamu.

Kaimu Mkurugenzi wa divisheni ya Katiba na Haki za Binadamu Ofisi ya Mwanasheria Mkuu Bi. Alesia Mbuya amesema hayo leo Jijini Dar es Salaam wakati ofisi yake ikitoa taarifa ya mrejesho wa mapendekezo ya mkutano wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa kwa mwaka huu na nafasi ya nchi kukabiliana na mapendekezo hayo.

Aidha, ofisi hiyo kupitia kwa Mkurugenzi Msaidizi wa Masuala ya Haki za Binadamu imesema kuwa masuala yeyote yanayoonesha kunyanyaswa kwa mashirika yasiyo ya kiserikali nchini Tanzania hasa wakati wa uchaguzi hayakutajwa, licha ya kukiri kuwa Umoja wa Mataifa umeitaka nchi kulinda haki za watu wenye ualbino.