Jumatatu , 7th Dec , 2015

Serikali ya mkoa wa Katavi imemsimamisha kazi mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Mpanda na maafisa wengine wa Halmshauri hiyo ili kupisha uchunguzi dhidi ya ubadhirifu wa miradi mbalimbali ya wilaya hiyo.

Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt Ibrahim Msengi

Akizungumza mara baada ya kikao cha kamati ya usalama ya mkoa, mkuu wa mkoa wa Katavi Dkt. Ibrahim Msengi amesema maafisa hao wamesimamishwa kutokana na kubainika kwa ufisadi katika maeneo tofauti.

Dkt. Msengi amesema kuwa maafisa hao pamoja na mkurugenzi hawataruhisiwa kutoka nje ya mkoa huo mpaka pale uchunguzi utakapokamilika ili hatua za kisheria zichukuliwe kwa watakaobainika kuhusika moja kwa moja.

Aidha mkuu huyo wa mkoa ametoa onyo kwa watumishi wote wa mkoa wa Katavi kuwa serikali haitasika kuchukua hatua kwa yoyote atakayehusika na ubadhrifu na kwamba waliozoea kufanya hivyo basi wajue mwisho wao umefika.