
Rais wa (EAAACA) wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa kwa nchini za Afrika Mashariki, Valentino Mlowola.
Hayo yamebainishwa na Rais wa (EAAACA) wa taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa kwa nchini za Afrika Mashariki, Valentino Mlowola ambapo amesisitiza kuwa kuwepo kwa baadhi ya halmashauri nchini kunaendeleza kudidimiza hali za wananchi suala ambalo bado wanalipinga vikali na kuhakikisha haki inapatikana kwa kila raia,na taasisi mbalimbali.
Mara baada ya kufungua mkutano huo Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angela Kairuki ametumia fursa hiyo kutoa wito kwa nchi za jumuiya hiyo kuhakikisha zinashirikisha taasisi binafsi katika kutokomeza rushwa sambamba na kurekebisha baadhi ya vipengele katika sheria ya kudhibiti rushwa.
Angela Kairuki
Aidha kwa upande wake Edward Nnko, ambaye ni mwalimu na msimamizi wa klabu ya kupinga rushwa katika Shule ya Sekondari Arusha ameeleza kuwa kuna umuhimu wa kuwajengea msingi kwa vitendo wanafunzi katika kupiga vita suala la rushwa licha ya kufundishwa darasani kwa baadhi ya masomo suala ambalo litasaidia kufikisha elimu kuhusu kudhibiti rushwa katika jamii.
Imeelezwa kuwa kwa nchi za Afrika Mashariki Tanzania ni nchi ya pili katika kutokomeza rushwa kwa maendeleo ya taifa.