Jumatatu , 29th Mei , 2023

Joyce Sengerema mwenye umri wa miaka 10 mkazi wa Kijiji cha Kiloleli wilayani Kishapu mkoani Shinyanga amejeruhiwa na Fisi wakati akienda kuchota maji mto Manonga majira ya saa 12:00 asubuhi na kisha kumburuza hadi vichakani.

Mtoto aliyejeruhiwa

Imeelezwa matukio ya fisi kuvamia makazi ya watu bado ni changamoto kubwa Mkoani Shinyanga ambayo inahitaji kupatiwa ufumbuzi wa haraka

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Kiloleli Edward Manyama, amesema matukio ya Fisi kuvamia makazi na kujeruhi pamoja na kubeba mifugo yamekuwa yakitokea mara kwa mara huku Muuguzi wa zamu Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga Jesse Samwel amesema mtoto huyo amepata majeraha kichwani na mkono wa kushoto.

Akizungumzia tukio hilo kwa njia ya simu Kamanda wa Jeshi la polisi Mkoa wa Shinyanga Janeth Magomi amesema wanashirikiana na wataalam wa wanyama pori kuwadhibiti fisi hao.