Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump baada ya kushambuliwa
Biden ametoa tamko hilo takribani saa mbili baada ya tukio hilo kutokea huku akisisitiza kuwa Marekani haiwezi kuruhusu na kuvumilia matukio kama hayo.
Rais wa zamani wa Marekani, Donald Trump ambaye tayari ametangaza nia kuwania tena Urais katika uchaguzi ujao wa Marekani, alilazimika kukatisha mkutano wake wa hadhara uliohudhuriwa na maelfu ya wafuasi wake baada ya shambulio hilo huku video na picha zikionesha akiwa na damu eneo la sikio.
Idara ya upelelezi nchini Marekani (FBI) imetoa taarifa za mtuhumiwa wa jaribio la mauaji ya Rais wa Zamani Donald Trump ambaye ametambulika kwa jina la Thomas Matthew Crooks mwenye Umri wa miaka 20.
Baadhi ya video zimemuonesha mtuhumiwa huyo aliyekuwa juu ya jingo ambapo baadhi ya mashuhuda wamekiri walimuona.