Jumanne , 20th Aug , 2024

Familia ya Imamu mstaafu wa Msikiti wa Tambaza uliopo Upanga jijini Dar es Salaam, yenye watu 21, imevunjiwa nyumba waliyokuwa wanaishi wakidai bila kupewa samasi ya Mahakama hali iliyozua taharuki kubwa huku wakiiomba Serikali kuwasaidia kupata haki Yao wanayoitafuta kwa zaidi ya miaka20.

Familia ya Imamu mstaafu wa Msikiti wa Tambaza yavunjiwa nyumba.

Akiongea na wana habari mama mwenye nyumba hiyo anasema nyumba hiyo ni makubaliano baina ya marehemu mume wake na aliyekuwa mmiliki wa eneo la Upanga, marehemu Mohamedi Tambaza.
"Wakati Msikiti unajengwa walikuwa wanatafuta Imamu kipindi hicho mume wangu anaishi kwao Pemba ikabidi wamsafirishe aje kuhudumu hapa na ndipo kwa makubaliano wakampa eneo la kiwanja namba 611, lakini akatolewa uimamu wakati huo tayari tulikuwa tunaishi hapa kwahiyo akaondoka kwenye eneo la mgogoro  cha ajabu leo tunatolewa wakati tulishinda kesi mara nne", Safisa Mohamedi, Mama mwenye nyuma.

"Madalali walituletea brua ya kuondoka eneo hili lakini hatukusaini kutokana na eneo linalotakiwa kuvunjwa ni jingine ambalo ni kiwanja namba 611, lakini sisi tupo kiwanja namba 580, kwahiyo tuliwaambia hatuwezi kusaini kwa sababu sisi hatumiliki kiwanda namba tajwa, cha ajabu leo tumeshangaa asubuhi tumevamiwa tunavunjiwa na kuibiw baadhi ya mali zetu", alisema Hudah Mohamedi, Mtoto wa mwenye nyumba.

"Kwanini familia ivamiwe bila kibali tumepiga simu Polisi hakuna msaada wowote mpaka sasa, tumevamiwa na wahuni ambao tunawaomba kibali au hati ya Mahakama inayosema kwamba hii nyumba ivunjwe hawana wanatuonesha tu kibali cha Polisi kuwapa ulinzi wanapotekeleza hili zoezi", alisema Saidi Kiwelu, Mjomba wa Familia iliyovunjiwa.

Mwanasheria wa familia ya Imamu Mstaafu, Wakili Yahya Njama anasema uvunjani huo haukufuata taratibu kwani nyumba inayovunjwa na iliyotakiwa kuvunjwa ni tofauti. 

EATV ikawatafuta uongozi wa Serikali ya Mtaa na alipopigiwa Mwenyekiti Joha Abdallah, akajibu kuwa zoezi hilo linatekelezwa na Kamanda wa Polisi, mkoa wa Kinondoni.

Hatukuishia hapo je, Diwani Adinan Kondo ana lipi kuhusu uvunjaji huo.
"Changamoto hiyo naijua lakini kwa mujibu wa nyaraka inaonesha familia hiyo ilipewa iishi kwenye eneo hilo kwa kipindi ambacho baba wa familia alikuwa imamu na nyaraka zilikuwa zinasema kuwa atakapoondoka atatakiwa aachie eneo hilo na hatakiwi kurithisha", alisema Kondo.