Rais jakaya Kikwete na Rais wa Zanzibar, Dk. Alli Mohamed Shein wakionesha Katiba hiyo iliyopendekezwa na Bunge Maalum la Mabadiliko ya Katiba.
Mtaalamu na Mtathmini wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu Bw. Castor Kalemela amesema leo kuwa, ni vema wananchi wakaelewa mambo ya msingi kwenye Katiba pendekezwa ili kuipigia kura.
Bw. Kalemela amesema, ni vema wananchi wakasoma na kuelewa vifungu vyote kwani Katiba ni chombo kinachosimamia maisha ya Taifa kwa ujumla.
Bw. Kalemela amelitaka pia kanisa kusimama imara na kutokuwa dhaifu kutokana na kundi linalotoa vitisho kuhusu viongozi wa dini wanaojiingiza katika siasa.
Naye Bw. Akida Majenga Mwanasheria wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu amesema, licha ya mchakato kuhusisha wananchi ila kuna mambo ambayo yamepunguzwa kwenye Katiba Pendekezwa.
Hata hivyo, Bw. Kalemela amepongeza, kwa mara ya kwanza serikali imeshirikisha wananchi katika kutoa maoni na mapendekezo yao na kufanyiwa kazi hadi kupelekea mchakato huo kufanyika.