Jumanne , 30th Mei , 2023

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Stergomena Tax amesema Wizara ipo katika hatua za mwisho za maandalizi ya kuwapatia Hadhi Maalum Diaspora wenye asili ya Tanzania na Uraia wa nchi nyingine (Tanzania Non-Citizen Diaspora)

Kauli hiyo ameitoa wakati akiwasilisha Bungeni Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 ambapo amesema Wizara ilikusanya maoni toka kwa Wadau mbalimbali ndani na nje ya Nchi, ikiwa ni pamoja na kutoka kwa Diaspora wenyewe

“Maoni yameainisha maeneo/masuala yanayopendekezwa kujumuishwa katika Hadhi Maalum, aidha mwezi Machi 2023, Serikali kupitia Benki Kuu ya Tanzania ilitoa maelekezo kwa Benki na Taasisi za Fedha Tanzania kuruhusu Raia wa kigeni wakiwemo Diaspora wenye asili ya Tanzania na uraia wa Nchi nyingine kufungua akaunti za fedha za kigeni kwa kutumia vitambulisho mbadala vya utambuzi tofauti na hati ya kusafiria ya Tanzania na kitambulisho cha NIDA” amesema Waziri Tax