
DCI Ramadhan Kingai (Katikati), wakati akizungumza na Maafisa wa Jeshi la Polisi
Hayo ameyasema leo Agosti 9, 2023 alipofanya kikao kazi na Askari wa vyeo mbalimbali wa Mkoa wa Kipolisi Rufiji.
Amewataka Maofisa, Wakaguzi na Askari wawafikishie elimu hiyo wananchi ili watambue kwamba upelelezi unatakiwa ufanyike kabla ya mtuhumiwa kukamatwa.
Na kwamba pindi mtuhumiwa anapopatikana au kukamatwa wapelelezi waandae jalada ili lipelekwe katika Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka kwa ajili ya kuandaa hati ya mashtaka ili mtuhumiwa afikishwe mahakamani.