Jumatatu , 21st Apr , 2025

Kijana David Kahela, anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 29 mkazi wa Mtaa wa Makutano, amekutwa amefariki dunia katika mtaa wa Mhama, Kata ya Malangali, Manispaa ya Sumbawanga mkoani Rukwa.

Mwili wa David Kahela

Taarifa za kifo hicho zimethibitishwa na Mwenyekiti wa Mtaa huo, Silasi Kayange pamoja na ndugu wa marehemu, Godfrey Kahela ambaye ni kaka wa marehemu.

Kwa sasa chanzo halisi cha kifo hicho bado hakijajulikana, na Jeshi la Polisi limechukua mwili wa marehemu kwa ajili ya uchunguzi wa kina ili kubaini sababu kamili zilizopelekea kifo hicho.

Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi wake na limewataka wananchi kuwa watulivu huku likifuatilia kwa ukaribu tukio hilo la kusikitisha.