Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari ni kwamba mtambo wa Ruvu Chini utazimwa ili kuruhusu mkandarasi kuunganisha bomba jipya na bomba la zamani katika tanki la Maji Wazo - Tegeta.
Zoezi hili linaashiria kuanza kukamilika kwa upanuzi wa mtambo wa maji wa Ruvu Chini ambapo shirika linakusudia kuzalisha maji mapya toka kiwango cha sasa cha cubic za ujazo 182,000 hadi cubic 270,000 kwa siku kuanzia mwezi Februari 2016 na kuondoa kabisa tatizo la maji kwa maeneo yanayohudumiwa na mtambo wa Ruvu
Maeneo yatakayoathirika yafuatayo ni kama ifuatavyo Bagamoyo, Bunju, Boko, Tegeta, Kijitonyama, Kinondoni, Kunduchi, Osterbay, Magomeni, Upanga, Kariakoo, katikati ya jiji, Ilala, Ubungo, Kigogo, Mburahati, Muhimbili, Buguruni, Changombe, Mbezi beach, Jangwani, Salasala, Mlalakuwa, Mwenge, Kigogo, Sinza, Msasani, Mikocheni na Keko.
Aidha DAWASCO imewataka wananchi kuhifadhi maji ya ziada ya kutumia ili kuepuka usumbufu utakaojitokeza.