Jumatano , 15th Feb , 2023

Wamiliki na madereva wa daladala jijini Mwanza wamesema watasitisha kutoa huduma ya usafiri kwa wakazi wa jiji hilo kufuatia uwepo wa bajaji mjini zinazobeba abiria katika vituo vya daladala na kupelekea wao kushindwa kufanya kazi.

Daladala

Hayo yamebainishwa kwenye kikao maalum kilichowakutanisha madereva wa daladala, pikipiki na bajaji pamoja na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA), kikao ambacho kimelenga kusikiliza changamoto walizonazo madereva na kuzitafutia ufumbuzi ambapo madereva wa daladaa wamesema uwepo wa bajaji mjini pamoja na faini za makosa ya barabrani umepelekea wao kufilisika.

Zakayo Mashamba ni dereva bajaji naye akazungumza kuhusu malalamiko yaliyotolewa na wamiliki na madereva wa daladala.

"Wanaoendesha hiache na costa nashukuru leo wamekuwa wawazi tulikuwa tunaona wanazirusha bajaji tulikuwa hatujui kumbe kuna namna, nashukuru leo tumejua, wote sisi ni Watanzania mipaka haiongezeki lakini watu wanaongezeka sasa sisi watu wa bajaji tukale wapi?," amehoji Mashamba.

Wakijibu malalamiko ya wamiliki na madereva wa daladala Mkurugnezi wa Huduma za Uchukuzi kutoka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi Aron Kisaka, pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa LATRA Habibu Suluo, wamesema kama madereva wa bajaji wanapakia abiria kwenye vituo vya daladala wanafanya makosa