Jumamosi , 10th Feb , 2024

Daktari tarajali wa Hospitali ya Rufaa Sokoine na Mkazi wa Mtaa wa Mtanda Wilaya ya Lindi, baada ya kukiri makosa na kulipa faini ya Shilingi 1,000,000/= au kwenda jela mwaka mmoja, kwa makosa ya kushawisi na kupokea hongo ya Shilingi 70,000/=.

Hukumu hiyo dhidi ya Isaya Makali Lucas katika shauri la jinai Na. 03/2024, imetolewa chini ya Mhe. Maria Batulaine – Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Lindi Febuari 7, 2024.

Mshtakiwa huyo alipokea hongo ya Shilingi 70,000/= kutoka kwa ndugu wa mgonjwa Bw. Yusufu Hamisi Juma, ambaye alikua anamuuguza Bw. Saidi Omari Nyanyari.

Hata hivyo Mshtakiwa huyo amelipa faini ya TZS. 500,000/ = kwa kila kosa na kuachiwa huru.