
Chama cha wafanyakazi wa sekta ya mawasiliano na uchukuzi nchini Tanzania (COTWU) kimewataka waajiri kufanya kazi zao kwa kuzingatia sheria ili waweze kupunguza migogoro inayoonekana kuongezeka katika maeneo ya kazi.
Akiongea na waandishi wa habari Mwenyekiti wa chama cha (COTWU) Idrisa Washington amesema kuwa utafiti wao umebaini kuwa migogoro mingi inayotokea sehemu za kazi inasababishwa na waajiri kutozingatia sheria na michache husababishwa na viongozi wa vyama vya wafanyakazi ambao hupenda kumaliza migogoro yao kwa malumbano.
Katika hatua nyingine chama hiko kimejiandaa kufanya mkutano mkubwa mwezi July mkutano ambao unalenga kuwajadili viongozi waliosimamishwa kazi kwa kuhusishwa na upotevu wa zaidi ya shilingi milioni 120.
