![](http://eatv.tv/sites/default/files/styles/detailpageimg/public/field/image/kamani_1.jpg?itok=-4JTN_Wu×tamp=1472594521)
Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dkt Titus Kamani
Akizungumza kwa njia ya simu na HOT MIX, Kaimu Mkuu wa chuo hicho, Joseph Kasiga amesema kuwa mfumo wa kutoa vyeti katika vyuo vya mifugo nchini umebadilika ambapo kwa sasa wanafunzi hao wanapata vyeti kwa kila muhula wanaosoma hali ambayo wanafunzi wa vyuo hivyo hawajakubaliana nao.
Amesema kuwa wanafunzi hao walianzisha mgomo baridi wa kuingia madarasani lakini leo wameamua kufunga milango ya madarasa pamoja na ofisi za walimu pamoja na geti la kuingilia chuoni hapo kwa makufuli mapya hali iliyowalazimu viongozi wa chuo hicho kuwasiliana na uongozi wa Wilaya kuwaelezea hali ilivyo chuoni hapo.
Amesema baada ya kuwasiliana na Wizara ya maendeleo ya mifugo na uvuvi waliamuru chuo hicho kufungwa kutokana na kuwepo viashiria vya uvunjifu wa amani chuoni hapo.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya hiyo Dk, Jasmin Tiisekwa amesema kuwa chuo hicho kina jumla ya wanafunzi 539 ambao wote waliamuriwa kutawanyika katika eneo la chuo hicho ndani ya saa mbili.
Polisi waliimarisha ulinzi katika chuo hicho na hakuna miundombinu yoyote iliyoharibiwa.