Jumatatu , 20th Mar , 2023

Rais wa China Xi Jinping yuko mjini Moscow kwa ziara ya siku mbili na mazungumzo na Rais wa Urusi Vladimir Putin. 

 

Hii ni ziara ya kwanza ya Xi nchini Urusi tangu wanajeshi wa Urusi walipoivamia Ukraine mwaka 2022. Rais huyo  anatarajiwa kupata chakula cha mchana na Putin baadaye, na kufanya mazungumzo rasmi Jumanne.

Ziara hiyo inafanyika siku chache baada ya Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) kutoa waranti wa kukamatwa kwa Rais Putin kwa madai ya uhalifu wa kivita. Beijing imeielezea kama ziara ya urafiki na amani, huku Urusi ikisema viongozi hao watajadili ushirikiano kamili na ushirikiano wa kimkakati.

Mwezi uliopita Beijing ilitoa mapendekezo ya kumaliza vita nchini Ukraine, ambapo nchi za Magharibi zimetoa mapokezi ya vuguvugu Awali mataifa ya Magharibi yaliionya Beijing dhidi ya kuipatia Moscow silaha.

Madai hayo yanakanushwa na china.