Jumanne , 16th Mei , 2023

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, amefanya ziara ya kushtukiza katika soko la Mwenge ikiwa ni mara yake ya kwanza kufanya hivyo baada ya kuhamishiwa akitokea mkoani Kagera.

Albert Chalamila alipokuwa Mwenge sokoni

Chalamila amefanya ziara hiyo leo Mei 16, 2023 ikiwa ni siku moja tangu Rais Samia Suluhu Hassan alipofanya mabadiliko madogo ya wakuu wa mikoa na hivyo kumuhamisha kutoka mkoani Kagera alikohuduma kwa zaidi ya miezi sita.