Jumatano , 17th Dec , 2014

Chama cha Demokrasia na Maendeleo - CHADEMA kimeitaka serikali kuwachukulia hatua ikiwemo kuwafikisha mahakamani viongozi waliohusika katika wizi wa fedha katika akaunti ya Tegeta - Escrow - licha ya wengine kuandika barua kujiuzulu.

Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA (bara), Mhe. John Mnyika

Akizungumza na waandishi wa habari, Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA (bara), Mhe. John Mnyika amemtaka Rais Jakaya Kikwete kuyafanyia kazi maazimio ya bunge ya kuwaondoa na kuwafikisha katika vyombo vya sheria viongozi hao, hata kama watajiuzulu nyazifa zao.

Akielezea uchaguzi wa serikali za mitaa, Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Zanzibar Bwana Salum Mwalimu amemtaka waziri wa TAMISEMI Mhe. Hawa Ghasia kutangaza matokea chaguzi za serikali za mitaa kwa nchi nzima badala ya kuwaachia viongozi wa vyama vya siasa kuendelea kuwadanganya wananchi kuwa vyama vyao vimepata ushindi wa kishindo.

Kwa upande wao baadhi ya wananchi wameitaka serikali kufuatilia ajira za wageni katika baadhi ya benki nchini kutokana na ongezeko la wizi ambao unaambatana na baadhi ya watendaji kujiuzulu nyadhifa zao baada ya muda.