Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimedai kuwa ofisi za watendaji wa Mitaa, Vijiji na Vitongoji zimefungwa kuanzia Bukoba Vijijini, Dar es salaam, Simiyu, Solwa, Bariadi na maeneo mengine nchini.
Taarifa ya Chadema iliyotolewa na Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya nje John Mrema imeeleza kuwa Chadema wanaitaka TAMISEMI ielekeze Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi wawepo ofisini ili kupokea mapingamizi yao.
Aidha Chadema imeitaka TAMISEMI ifungue mlango mwingine wa kupokea mapingamizi ikiwa watendaji wataendelea kukaidi amri ya kuwa ofisini
Pamoja na hayo Chadema wameitaka TAMISEMI kuchukua hatua za kinidhamu dhidi ya Watendaji na Wasimamizi wote ambao wanaharibu Uchaguzi Kwa makusudi huku wakijua kufanya hivyo kunaweza kulitumbukiza Taifa kwenye machafuko.
Chadema imewasisitiza Wanachama, Wagombea na Viongozi wao wa maeneo yote walioenguliwa, wakate rufaa na kwenda kuziwasilisha kwenye ofisi za watendaji na kama zimefungwa ofisi hizo wakae hapo mpaka ofisi zitakapofunguliwa na watendaji kupokea mapingamizi yao. #EastAfricaTV