Alhamisi , 16th Mar , 2023

Halimahauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Ilala Mkoani Dar es salaam imeeleza kuridhishwa na utekelezaji wa Ilani Cha chama hicho Kwa kipindi Cha kuanzia mwezi juni Hadi Disemba mwaka 2022 ambapo katika kuelekea miaka miwili ya Rais DKT Samia Suluhu Hassan wana imani kubwa.

Rais wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan.

Akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kikao hicho ya kupokea taarifa ya utekelezaji wa ilani ya CCM Wilaya Ilala Mwenyekiti wa chama hicho Wilaya ya Ilala Said Side amesema Ilani imetekelezwa kikamilifu Kwa kipindi Cha kuanzia mwezi juni Hadi Disemba mwaka 2022.

Sambamba na hilo Halmashauri kuu ya CCM Wilaya ya Ilala Imeeelekeza kuondolewa Kwa Wakandarasi wasio na uwezo wa kutekeleza miradi Kwa wakati na kuishauri wasipatiwe kazi nyingine mpaka watakaookidhi viwango.

Akiwasilisha utekelezaji wa Ilani Kwa niaba ya Mkuu wa wilaya ya Ilala Katibu Tawala wilaya hiyo Charangwa Selemamn amesema Kwa kipindi hicho wameimarisha maeneo yote muhimu ikiwemo sekta ya Elimu, miundombinu afya na utalii

Wakati huohuo Halimashauri ya Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Ilala imeielekeza Ilala kuhakikisha inaongeza zaidi vyanzo vya mapato ilibkuendelea kuwahudukia wananchi Pamoja na mambo mengine kikao hicho kimeshauri kuendeleza umoja na mshikamano Kwa maendeleo ya taifa