Wananchi na wanafunzi wa shule ya sekondari Lukuvi wakishiriki kuzima moto katika bweni la wanafunzi lilipoungua kwa Mara ya Kwanza.
Kaimu Kamanda Pundensiana Protas amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambaopo amesema hakuna mtua ambaye ameathirika kutokana na ajali hiyo.
Kaimu Kamanda amewataka wananchi na wamiliki wa taasisi kuchunguza miundombinu ya umeme katika nyumba zao ili kuepukana majanga ya moto.
Aidha, Bibi Pudensiana amesema jeshi la polisi bado linachunguza chanzo cha ajali hiyo.
Ajali hiyo ya moto ni mara ya pili katika shule ya Sekondari ya William kwani ajali ya awali imetokea Mei 11 mwaka huu kutokana na hitilafu ya umeme wa sola.