Jumanne , 11th Oct , 2022

Zaidi ya kaya 300 katika kijiji cha Mnadani katika Halmashauri ya wilaya ya Iringa  zilizopo ndani ya hifadhi ya bwawa la Mtera zimetakiwa kuhama ili kunusuru bwawa hilo ambalo liko hatarini kutoweka kutokana na kuathiriwa na shughuli za kibinaadamu ikiwemo kilimo

Bwawa la mtera limekuwa tegemeo kwa wakazi wa halmashauri za wilaya ya iringa, chamwino na Mpwapwa kwa ajili ya kufanya shughuli za uvuvi na kuendesha miasha yao lakini changamoto kubwa kwasasa bwawa hilo maji yake yanazidi kupungua na samaki kutoweka kutokana na wananchi wanaozunguka bwawa hilo kufanya shughuli za kilimo pembezoni mwa bwawa hilo

Lakini katika kunusuru bwawa hilo  Tume ya taifa ya mipango ya matumizi ya ardhi kwakushirikiana na ofisi ya makamu wa rais Mazingira  imeanza  utekelezaji wa  mradi wa uhifadhi wa vyanzo vya maji kwenye vijiji vya makuka ,makatapola na mnadani wilayani iringa ambavyo  vinavyozunguka bwawa hilo

Lakini wananchi wanapokeaje mpango huo wa urasimishaji wa ardhi unaoratibiwa  na tume ya taifa ya mipango ya matumizi ya ardhi?