Ijumaa , 3rd Jul , 2015

Miswada mitatu ya Mafuta na Gesi imeshindwa kusomwa tena kwa mara ya pili hii leo baada ya spika wa Bunge bi, Anne Makinda kulazimika kuahirisha kikao kutoka na wabunge wa upinzani kuanza kuzomea kupinga uwasilishwaji wa misawada hiyo.

Spika wa Bunge la Jamhuri la Muungano wa Tanzania Bi. Anne Makinda akisisitiza Jambo Bungeni.

Baada kupitisha Muswada wa sheria ya kuwalinda watoa taarifa za uhalifu na mashahidi Spika Makinda alimwita Waziri wa Nishati na Madini aweze kutoa hoja juu ya miswada iliyotakiwa kuwasilishwa leo ndipo wabunge walipotaka kutoa miongozo ambayo spika aliipinga.

Wakati Waziri wa Nishati na Madini Mh. George Simbachawene alipoanza kusoma Mswada sheria ya usimamizi wa mapato ya mafuta na gesi 2015 , wabunge wakaripuka kwa kelele na kuanza kuzomea kitendo kilichomlazimu Spika makinda kusitisha kuendelea kwa kikao hicho.

Hapo awali baada ya kipindi cha Maswali na majibu mbunge wa Ubungo alitoa hoja ya kutaka misawada hiyo ya mafuta na gesi iliyoletwa kwa hati ya dharura na badala yake wajadili changamoto zinazolikabili zoezi la uandikishaji daftari la mpiga kura pamoja na uchaguzi mkuu.

Aidha Spika makinda amewaita baadhi ya viongozi wa upinzani akiwemo Mh. Tundu Lisu, John Mnyika, Habib Mnyaa, David Silinde, Rashid Abdallah, Moses Machali kukutana kamati ya maadili ya Bunge ili kujadili tukio hilo la leo.