Jumanne , 20th Mei , 2014

Kambi ya Upinzania Bungeni imeitaka Serikali kuweka sheria zinazo walinda na kuwapendelea wawekezaji wazawa katika sekta ya uwekezaji wa rasilimali za taifa ikiwa ni pamoja na sekta ya mafuta na gesi.

Baadhi ya wachimbaji wadogo wadogo wakiwa kazini katika moja ya mikoa ya kanda ya ziwa nchini Tanzania.

Akitoa mapendekezo ya Kamati ya Bunge ya Viwanda na Biashara, ya Makadirio ya Bajeti ya Wizara ya Viwanda na Biashara kwa mwaka wa fedha 2014/2015 Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Luhaga Mpina amesema serikali ina wajibu wa kuwasaidia wawekezaji wazawa kwa kuwapa mitaji pamoja na kuwaendeleza kiteknolojia katika sekta hiyo ili kunufaika.

Kwa upande wao, wabunge Ciril Chami, Margret Mkanga pamoja na Said Musa Zuberi wakichangia bajeti hiyo wamesema serikali iwekeze zaidi katika viwanda ikiwa ni pamoja na kuingia mikataba ambayo serikali itapata asilimia kubwa ya faida kuliko wawekezaji.