Jumatano , 30th Mar , 2022

Wanafunzi watatu wa familia moja wanaosoma shule ya msingi Bukoli, wawili darasa la tatu (10) na mmoja darasa la kwanza (8), iliyopo wilaya ya Geita mkoani Geita wanadaiwa kulawitiwa kwa nyakati tofauti na kaka yao binamu mtoto wa shangazi yao anaejishughulisha na uchimbaji mdogo.

Makao Makuu ya Jeshi la Polisi mkoa wa Geita

Mwalimu wa Afya shule ya msingi Bukoli, Mosses Luheja amesema baada ya kuona mtoto ametokwa na utumbo kwenye njia ya haja kubwa wakamkimbiza kituo cha Afya Bukoli anasema baada ya kumfanyia uchunguzi mototo huyo akagundua ameingilia kinyume na maumbile.

Jeshi la Polisi mkoa wa Geita bado linaendelea na uchunguzi juu ya tukio hilo.

Tazama Video hapo chini