.jpg?itok=HSp76fxa×tamp=1478625275)
Wateja wakigombania kuingia ndani ya benki ya Twiga, Makao Makuu mtaa wa Samora jijini Dar es Salaam hii leo.
Meneja Msimamizi ambaye Benki Kuu imemteua kusimamia uendeshaji wa benki hiyo Bw. Nkanwa Magina, amewaambia waandishi wa habari kuwa kwa sasa benki hiyo itatoa huduma muhimu huku baadhi yake zikisitishwa kwa muda kwa kipindi cha mpito ambacho hata hivyo hakusema kitachukua muda gani.
Kwa upande wake, Afisa Mtendaji Mkuu wa Umoja Switch inayosimamia mtandao wa ATM ambako huduma za Twiga Bancorp pia inapatikana Bw. Danford Mbilinyi amesema kwa agizo la Benki Kuu wamefungulia huduma za benki hiyo na kwamba sasa zinapatikana kama kawaida.