Jumatatu , 26th Sep , 2016

Benki Kuu ya Kenya (CBK) imebainisha kuwa mabenki nane kutoka nchi za kigeni zinajiandaa kuingia katika soko la Kenya licha ya kuwekwa kiwango cha ukomo wa riba na mamlaka hiyo.

Gavana wa Benki Kuu ya Kenya, Partick Njoroge.

Gavana wa Benki Kuu ya Kenya, Parick Njoroge, amesema kuwa mabenki yamekuwa yakivutiwa na mzunguko mkubwa wa fedha nchini humo pamoja na hali ya kijiografia inayofanya kuwa ni eneo la kuingilia soko la Afrika.

Gavana Njoroge amesema kuwa benki ambazo zinataka kuwekeza kwenye mipaka ya Kenya miongoni mwao ni kutoka Japan, kufuatia mkutano wa TICAD, Marekani, Umoja wa Falme za Kiarabu na Afrika Kusini.