Zaidi ya wakazi 500 wa vijiji vinavyozunguka mgodi wa North Mara ulioko Nyamongo wilaya ya Tarime mkoani Mara wameathirika na milipuko ya baruti iliyopigwa mgodini na kusababisha madhara ikiwemo mabati ya nyumba kutoboka na baadhi ya wananchi kujeruhiwa .
Wakizungumza kwa uchungu wananchi walioathiriwa na milipuko ya baruti iliyolipuliwa ndani ya mgodi wa nyamongo wametupia lawama serikali kutowachukulia hatua wawekezaji hao licha ya madhara yaliojitokeza kwa wananchi ikiwemo baadhi ya nyumba kuharibika baada ya mabati kutobolewa na mawe na kuomba serikali kutenda haki.
Kwa upande wake mwenyekiti wa serikali ya kijiji cha mijini kati Bageni Isack amesema baada ya kutokea maafa hayo amewasiliana na uongozi wa mgodi lakini hakupata ushirikiano ambapo ameiomba serikali kuingilia kati kuwasaidia wananch wanaoishi jirani na mgodi kuwahamisha wananchi kwa kuwalipa fidia zao kwa madhara wanayoyapata.
Nae mgombea ubunge jimbo la tarime vijijini kwa tiketi ya chadema john heche amesema anashangazwa na hatua ya serikali kushindwa kuwahamisha wananchi wanaozunguka mgodi huo